Saturday, November 10, 2012

‘FABAK FASHIONS’, KHANGA ZA KALE SHOW @ SERENA – NOVEMBA 23

 
Mama wa Mitindo nchini Tanzania, Asia Idarous kupitia Kampuni yake ya Fabak Fashions wanakuletea onyesho kubwa la Khanga za Kale litakalofanyika Novemba 23, 2012 katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.....

Onyesho hili kubwa ambalo limekuwa likifanya vizuri kwa takribani miaka minne sasa na kupata mafanikio makubwa ndani na nje ya Tanzania hasa katika nchi ya Marekani, litawakutanisha wabunifu zaidi ya 30 kutoka nchi mbalimbaliambao wataonyesha mavazi yao waliyoyabuni.
Watu maarufu hapa nchini watapanda jukwaani siku hiyo kuonyesha mavazi ya khanga za kale kutoka kwa mama wa mitindo, Asia Idrous Khamsin ambapo fedha itakayopatikana kutona na onyesho hilo imepangwa kupelekwa katika kituo cha watu walioathirika na madawa ya kulevya kilichopo Kikale, wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani.

0 comments:

Post a Comment