Friday, October 19, 2012

"Wasanii wa Bongo Wana Maisha ya Maigizo" - Hermy B

 

WAKATI wasanii wengi Tanzania maisha yao ya nje yakionekana kuwa juu kifedha kumbe hali yao ni ngumu sana kimaisha, producer mahiri na mmiliki wa studio za B hitz mtu mzima Hermy B, amefuguka na kidai kuwa wasanii bado wana maisha magumu sana ambayo hayana mfano huku wengine wakiendelea kuazimana nguo na kubanana kwenye vyumba vya kupaga kama kuku.


Hermy B, alidai kuwa maisha ya nje ya wasanii wengi unaweza kusema ni watu ambao wanaishi kwenye starehe lakini bado hali ni ngumu na hii inatokana na uzembe wao wa kutofanya kazi kwa umakini na juhudi kwani wengi wakishakuwa na majina kidogo starehe ndizo zinazowamaliza.

Producer huyo alifunguka mambo mengi ikiwemo la kushuka kwa muziki wa kizazi  kipya ambapo alidai kwa kutokana uwepo wake ndani ya tasnia hiyo kwa miaka mingi aliweka wazi kuwa muziki unashuka siku hadi siku na hii inatokana na wasanii wenyewe kwani hawana mbinu mbadala za kuufanya muziki usonge na uendelee kutamba, wengi wapo kwa ajili ya kutafuta umaarufu na kuuza sura.

“Ni wasanii wachache sana wanaoishi maisha mazuri wengi bado wanaendelea kuishi maisha ya kifukara, kitu cha ajabu sana kwa msanii anayeheshimika mtaani kuishi maisha hayo magumu,” alisema.

0 comments:

Post a Comment