WASANII wengi wa tasnia
mbalimbali wanaojihusisha na bifu kwa lengo kukuongeza umaarufuru, mkali
asiyepotea ndani muziki wa bongo fleva Mwana FA,
ameamua kuweka wazi kuwa muziki bila bifu inawezekana na msanii anayeamini
kuwa bifu linamkuza kimuziki anapotea kwani umaarufu unakuja kutokana na
kazi nzuri zinazoelimisha na kuburudisha jamii na si vinginevyo.
Wapo wasanii wengi ambao mara
zote wamekuwa wakitengeneza bifu kwa madai kuwa wanaongeza umaarufu huku
wakisahau kuwa kazi nzuri ndiyo njia inayoweza kukuweka karibu na
mashabiki na si malumbano ambayo hayana maana yoyote.
Mtandao wa DarTalk,
ulifanya mazungumzo na msanii huyo ili kuzungumzia ishu na imani
zinasambaa mtaani kuwa bifu zinachangia kwa kiasi kikubwa kumtangaza
msanii, ndipo alipofuguka kuwa kwa upande wake haamini ishu hiyo
kwani anachojua kazi nzuri ndiyo jibu sahihi la kumweka juu mtu yeyote.
“Bifu si kitu cha kukipa nafasi
katika kazi kwani mara nyingi watu wanapoteza muda kwa sababu ya ishu
zisizokuwa na msingi, lakini kwa upande wangu nafanya muziki na sihitaji
kupoteza muda kwa sababu ya mtu fulani kwani najua madhara yake ni
mengi kama kunichafua na mashabiki wangu naweza kuwaweka njia panda,” alidai.
0 comments:
Post a Comment