Mkurugenzi wa shindano hayo, Methuselah Magese akizungumza
mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani).
SHINDANO la kusaka wanamitindo wenye vegezo vya kipekee nchini, linaloratibiwa na kampuni ya Unique Entertainment, leo limezinduliwa rasmi katika hoteli ya Holiday Inn Posta jijini Dar es Salaam.
SHINDANO la kusaka wanamitindo wenye vegezo vya kipekee nchini, linaloratibiwa na kampuni ya Unique Entertainment, leo limezinduliwa rasmi katika hoteli ya Holiday Inn Posta jijini Dar es Salaam.
Magese (katikati) akiwa pamoja na bodi yake ya
uandaaji
Shindano
la kumsaka mwanamitindo mwenye vigezo vya kipekee nchini Tanzania (unique
model) linaloandaliwa na Unique Entertainment limezinduliwa leo jumatano kwa
kishindo katika hoteli ya Holiday Inn iliyopo katika ya jiji la Dar es salaam
mbele ya waandishi wa habari....>>>
Akizungumza
na waandishi wa habari hao katika ufunguzi huo mkurugenzi wa shindano hilo Bw.Methuselah Magese amesema
kuwa mchakato wa shindano umefunguliwa rasmi ili kutoa fursa ya wadhamini
kujitokeza kwa wingi kudhamini shindano hilo ambalo litakuwa na mvuto wa aina
yake kwa msimu huu wa pili.
Pia
wanamitindo wenye sifa za kimataifa wameombwa kujitokeza kwa wingi katika
usaili utakaofanyika tarehe 18 novemba katika hoteli ya Lamada Apartments.
Tumeboresha
shindano kwa kiwango cha hali ya juu tofauti na ilivyokuwa hapo awali,lengo ni
kulifanya shndano hili liwe la heshima,hadhi na linalotimiza lengo lake la
kuvumbua na kuinua vipaji vya wanamitindo wa kchipikizi.
“Tunaomba
wabunifu wadogo kwa wakubwa wajitokeze kuja kuonyesha umahili wao katika
shindano hili ambapo mwaka huu tutakutanisha wabunifu wengi wa mavazi nchini
Tanzania katika shindano moja kwa lengo la kuwainua wabunifu wadogo na
kuendelea kuwatangaza wabunifu wenye majina makubwa katika tasnia ya mitindo
hasa katika kipindi hiki maridhawa cha mwisho wa mwaka” alisisitiza Magese.
Katika
msimu huu wa pili wa unique model kutakuwa na nyongeza ya mataji mengine madogo
matatu amabayo ni “model photogenic 2012”,”model talent 2012” na “model with
good manner 2012” ambapo mataji hayo yatakuwa chini ya taji kuu la “Unique
model of a year 2012”.
Fainali
za shindano la Unique model 2012 zitafanyika mwishoni mwa mwezi Desemba ambapo
kamati ya maandalizi imedhamilia kufanya onyesho lenye hadhi kuanzia ubora wa
washiriki wenye vigezo vya uanamitindo ambao wataleta mabadiliko katika tasnia
ya mitindo nchini.
Shindano
la Unique model lilianzishwa mwaka 2010 ambapo kwa mwaka huu ni mara ya pili
kufanyika, Asia
Dachi ndiye mwanamitindo anaeshikilia taji hilo mpaka sasa.
Wito
umetolewa kwa makampuni kujitokeza kuchukua mabalozi ambao ni wanamitindo
washiriki kwa lengo la kufanya nao kazi za kutangaza bidhaa ama huduma
inayotolewa na kampuni husika kwa lengo la kutoa ajira kwa wanamitindo hao
wanaochipukia katika tasnia.
Unique
model 2012 imedhaminiwa na DTV,Gazeti
la Tanzania Daima, Mashujaa investment ltd, Sophernner Investment co ltd, K.d.surelia, Young Don Records, Kiu investment ltd,Oriental Bureau De Change,100.5 Times fm, J’s professional ltd, Lamada Apartments Hotel, na Unique
entertainment Blog.







0 comments:
Post a Comment