Ni kitambo sasa tangu kuwepo kwa
taarifa kuwa staa wa Bongo Movie, Juma Kilowoko, 'Sajuki' ni mgonjwa ,
huku pia taarifa za karibuni zikidai kuwa hali ya nyota huyo
bado ni tete na kuzua hofu kubwa kwa mashabiki wake.
Kupitia teentz.com pekee taarifa
rasmi ni kuwa hali nyota huyo kwa sasa ni njema na yuko tayari
tena kuanza kuwatumikia watanzania kupitia tasnia ya
filamu.
Kwenye Exclusive interview aliyofanya
na teentz.com mapema leo Sajuki amewashukuru watanzania kwa kuwa pamoja
nae kwenye wakati wote wa matatizo mpaka sasa anajisikia yuko
vizuri tofauti na ilivyokuwa awali.
Nashukuru kuwa sasa niko poa,
watanzania waelewe hilo, kwa sasa naweza hata kuendesha gari na
karibuni nitaanza kucheza muvi tena alisema Sajuki.
katika kuonyesha kuwa anathamini
mchango wa Watanzania Sajuki ameachia ngoma ambayo ameamua kuipa jina la
Shukurani
Bonyeza Play kuisikiliza
Bonyeza Play kuisikiliza
NEW JOINT 'SHUKRANI' BY SAJUKI by Dismas Ten Slyvester







0 comments:
Post a Comment