Tuesday, October 30, 2012

BOB JUNIOR , "NIKO TAYARI KUSIMAMA NA DIAMOND"

 

Nyota wa ngoma ya ‘Nichumu’ ambaye pia  ni bosi wa lebo ya Sharobaro Record, ya  jijini Dar, Bob Junior amesema sasa yuko tayari kusimama kwenye ngoma  moja na mkali kutoka Wasafi Entertainments, Diamond Platinumz.
Akizungumza na teentz.com, mapema  leo  Bob Junior amesema licha ya kuwa aliwasiri jana jioni   kutoka  Oman alikokuwa kwa mapumziko na amepata bahati ya  kuisikiliza  ngoma  mpya ya Diamond na kuona kuwa  ni kawaida kwani haina kitu kipya ilichofanyiwa
"Unajua kwa sasa mimi nimewapisha vijana wangu kwanza  watoa ngoma zao na baada ya wiki mbili nitatoa ya kwangu, ninachoweza  kusema ni kuwa sasa niko tayari kusimama kwenye wimbo mmoja na dogo huyo kwani  naamini mimi ni mkali zaidi yake na watanzania  wanajua hilo" alisema  Bob.
Akiendelea zaidi Bob aliyeitikisa Bongo kwa  ngoma kali ya Oyoyo alifunguka kuwa, sasa ana mipango ya kufanya  vitu tofauti vitavyosukuma mbele muziki wa  kizazi kipya na zaidi akilenga  katika  kujiongezea mapato tofauti na kutegemea  MKWANJA WA shoo au promo za matangazo.

ALICHOKISEMA BOB JUNIOR KUHUSU UJIO WAKE MPYA by Dismas Ten Slyvester

0 comments:

Post a Comment