TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
SAFARI LAGER YATANGAZA KUKAMILIKA KWA MAFUNZO KWA WAJASIRIAMALI WA “WEZESHWA NA SAFARI LAGER”.
Dar es Salaam, Jumanne 24 April 2012:
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo
imetangaza rasmi kukamilika kwa mafunzo ya wajasiriamali waliopatikana
katika shindano la “Wezeshwa na Safari Lager”....>>>
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, Meneja wa bia ya
Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo alisema mafunzo kwa wajasiriamali wa “Wezeshwa na Safari Lager”
yalikamilika rasmi mwishoni mwa wiki katika mikoa ya Dar Es Salaam,
Arusha, Mwanza na Mbeya. Aliwapongeza wajasiriamali wote waliofaulu na
kupatiwa mafunzo haya yanayolenga kuwawezeshwa kupanua na kukuza
biashara zao. Akielezea mchakato wa kuwapata wajasiriamali hawa Bwana
Shelukindo alisema baada ya kutangaza kuanza kwa shindano hili mwishoni
mwa mwaka jana, jumla ya fomu za maombi 9,738 zilikusanywa. Fomu hizi
zilikaguliwa na majaji wenye ujuzi wa mambo ya biashara na wajasiriamali
80 walichaguliwa kuingia katika hatua ya pili. Wajasiriamali
waliochaguliwa walitembelewa na
wataalamu ili kuthibitisha uwepo wa biashara zao, jumla ya
wajasiriamali 54 walifaulu na ndio waliopatiwa mafunzo. Wajasiriamali 26
waliondolewa katika hatua hii kutokana na mapungufu mbalimbali kama
kuomba kuwezeshwa wakati biashara sio za kwao, kutokuwa na biashara
inayoendelea nk.
Shelukindo
alisema “Ni jambo jema kwamba wajasiriamali wetu wamepatikana kutoka
katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, wako wajasiriamali katika fani
tofauti pia kama Mafundi wa kushona nguo za aina tofauti, mafundi
seremala, magari nk wako pia wajasiriamali wa kusindika vyakula,
ufugaji wa samaki, ufugaji wa kuku, kutengeneza mizinga ya nyuki nk,
wako wajasiriamali katika biashara za vyakula, kuuza vinywaji, umeme
jua, teknolojia ya mawasiliano nk”.
Bwana
Shelukindo aliwataja wajasiriamali waliomaliza mafunzo na watapatiwa
ruzuku ya vitendea kazi ili kupanua biashara zao. Katika kituo cha Dar
Es Salaam wajasiriamali walifaulu ni Catherine Urio, Josephine Kisiri,
Zainabu Juma Zayumba, Elizabeth Chami, Richard Kwiligwa, Hilary Meck
Mremi, Damas Daniel Msoka, Innocent Mbelwa, Stumai Namanga, Martin
Richard Tupilike, Dasina J Buzuka, Christabela Lymo, Dadan J Munisi,
Faraji Bakary Mgwegwe, Issa Lema na Valerian Tigano Luzangi. Shelukindo
aliwataja pia washindi wa kituo cha Arusha kuwa ni Ansilla Danny, Bibie
Msumi, Rogers Msangi, Simon Kinabo, Sophia Khalfan, Yuda Mbando, Amani
Lymo, Adam Akilinyingi, Joseph M. Mnemwa, Rose Tesha na Victoria Riwa.
Bwana
Oscar Shelukindo aliendelea kuwataja wajasiriamali waliofaulu katika
kituo cha Mwanza ambao ni Bora Mganda, Brighton Dismas Maricell, Mangana
Kilahanya Kigombe, Prudence Mubito, Musa Mahushi George, Innocent K.
Doi, Amos Edward Mwambola, Edith Mudogo, Aron Magembe, Yusuph A. Kawaga,
Zamda Shabban, Oscar Bosco Kabobo, Yahaya Fundisa, Dainess Ngaiza na
Boniface Joseph Minja. Na katika kituo cha Mbeya wajasiriamali
waliofaulu kupata ruzuku baada ya mafunzo ni Rose Eliudi Maruila,
Benedict Abel Matandiko, Vumilia Mtweze, Bahati Mbata, Hellen A.
Mwanguku, Felix Phillip Kamuhabwa, Festo Mwakasege, Phares Richard Lymo,
Iradi A. Msemwa, Gabriel Mwalugaja na Tatu Ngemela. Jumla ya ruzuku ya
vitendea kazi vya thamani ya shilingi milioni 200 vitatolewa kwa
wajasiriamali
hawa.
Bwana
Shelukindo aliendelea kusema “Safari Lager tunayofuraha kubwa
kuwasaidia wajasiriamali hawa, tunawapa pongezi kwa uvumilivu wao na
jitihada kubwa waliyo nayo. Tutawakabidhi vitendeakazi vyao katika hafla
maalumu kuanzia wiki mbili zijazo”.
Akielezea
mafunzo yalivyoendeshwa Bw. Joseph Migunda wa taasisi ya TAPBDS alisema
wajasiriamali katika mikoa yote wameonyesha uelewa kwa kiwango cha juu
na wote walifaulu mtihani wa kuhitimisha mafunzo hayo. Alisema “Tuna
imani wajasiriamali watatumia elimu na ruzuku wanayopatiwa ili kupiga
hatua zaidi kufikia ndoto zao”.
Bwana
Shelukindo alimaliza kwa kuwashukuru watanzania wote kwa kushiriki
shindano hili, aliendelea “Shukrani nyingi sana ziende pia kwa wanywaji
wetu wa bia ya Safari Lager, bila wao hakika zoezi zima la Wezeshwa na
Safari Lager lisingewezekana, tunawaomba waendelee kufurahia bia yetu”.
Aliwaomba radhi wajasiriamali ambao hawakufaulu, na wale wanaoendelea
kutuma fomu wasitume tena, wajiandae kushiriki shindano lijalo la
Wezeshwa na Safari Lager baadae mwaka huu.
- - Mwisho - -
0 comments:
Post a Comment