Monday, August 27, 2012

Z-ANTO KUGONGA SHOW ZAMBIA



Msanii wa muziki wa kizazi kipya bongo, Z-anto, amenena kuwa amepata mualiko mkubwa wa Serikali ya Zambia kwenda kupiga show nchini humo Septemba 24, mwaka huu huku mgeni rasmi akiwa ni rais wa nchini hiyo .
Msanii huyo alisema kuwa mualiko huo ni kutokana na nchi hiyo huwa inasherekea sikukuu yao kila mwaka ingawa hajajua ni sikukuu ya aina gani ingawa kwa taarifa aliyopata ni kuwa siku hiyo wazambia wote huwa hawaendi kazini.
kwa sasa Z-anto yupo katika maandalizi ili aweze kuwawakilisha hata wasanii wengine wa Tanzania kwani anaamini safari hiyo haitakuwa ya pekee yake kwani nyuma yake atalibeba taifa la Tanzania.

“Yani ishu ambayo inanisumbua kichwa hapa ni juu ya maandalizi yangu ya safari ya kuelekea nchini Zambia kwa ajili ya kupiga show ambayo mwaliko wake ni mkubwa sana hiyo nawaomba watanzania waniombee niweze kujiandaa vizuri,” alisema.

0 comments:

Post a Comment