MKALI wa miondoko ya Taarab Hammer Q
ametangaza kujiunga rasmi na kundi linalofanya
muziki wa mduara la Offside Trick.
Hammer Q amesema amechukua uamuzi huo
wa kujiunga na kundi hilo baada ya msanii wa kundi hilo Muda Criss kupumzika
kufanya muziki, hivyo yeye kuziba nafasi hiyo.
Aliongeza kuwa mipango yake ya kumiliki
band bado iko palepale, na hata Offside Trick yupo kwa muda tu.
“Kwa sasa niko Offside Trick kwa muda
tu, kundi hili limenichukua ili niweze kuziba nafasi ya Muda Criss kwa kuwa
yeye ameamua kupumzika, na mipango yangu ya kumiliki band yangu binafsi bado
iko palepale” alisema Hammer Q.
Aidha aliongeza kuwa bado anaona ni
sawa kujiunga na wakali hao wa mduara kwa kuwa anaweza kufanya muziki wa aina
yoyote, kitu ambacho kinatofautisha kati ya msanii na mwanamuziki.
“Mimi ni mwanamuziki na sio msanii kwa
sababu naweza kuimba muziki wa aina zote, kwa hiyo hata kuwepo hapa Offside
Trick bado nafurahia” aliongeza.
Hammer Q amewahi kutamba kusikika
kupitia miziki ya aina ya tofauti ikiwemo aliyofanya kwa staili ya bongo fleva,
Taarab na mduara.
0 comments:
Post a Comment