Na Eleuteri Mangi- MAELEZO.
Wafanyakazi
Wizara ya Fedha wameaswa kufanyakazi kwa bidii na kujituma kwa moyo ili
kukuza uchumi wa nchi na taifa liweze kusonga mbele na kufikia malengo
yake.
Kauli
hiyo imetolewa na Mgeni Rasmi ambaye pia ni Waziri wa Fedha Saada Mkuya
Salum wakati wa kufungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa wizara
hiyo hivi karibuni jijini Dar es salaam.
“Mnapokuwa
kwenye mkutano wenu mjadili bajeti bila kuwa na woga kwa kutumia weledi
wenu mlionao na kutoa ushauri na maoni amabayo yatasaidia kujenga na
kuimarisha Wizara katika kutekeleza majukumu yake iliyojipangiakwa
kuzingatia uhalisia wa uchumi wa nchi” alisema Waziri Saada.
Katika
mkutano huo, Waziri Saada aliwapongeza wafanyakazi hao kwa kufuata
maelekezo ya kuwa na vikao vya baraza la wafanyakazi mara mbili kwa
mwaka kulingana na mkataba ambapo lengo lamkutano huo ni kupata
taafirifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2013/14 pamoja na kupitia na
kujadili bajeti ya mwaka 2014/2015.
Aidha,
mkutano wa baraza hilo unafanyika kwa kuzingatia agizo la Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete na katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Sefue kuitisha vikao kulingana na utaratibu
uliowekwa.
Naye
Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.
Servacius Likwelile akimkaribisha Mgeni Rasmi alisema kuwa mkutano huo
ndio una wajibu wa kupitia na kujadili bajeti ya mwaka uliopita na
mwaka ujao wa fedha ambapo bajeti ya Taifa itasomwa Juni 12, 2014.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima alisema kuwa moyo na
kiini cha hatima nchi ipo mikononi mwa watumishi wa Wizara ya Fedha,
hivyo ameahidi kuwa ofisi yake kwa kushrikiana na Naibu Waziri mwenzake
Mwigulu Nchemba ipo wazi wakati wote ili kuweza kusukuma maendeleo ya
nchi.
Akimshukuru
Mgeni Rasmi kwa niaba ya wajumbe wa mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu
Wizara hiyo Elizabeth Nyambibo alisema kuwa wajumbe wamemsikia na
watafanya kazi kwa bidii na kuwa wabunifu ikiwa ni pamoja na kuwapa
ushirikiano viongozi wao walioteuliwa na Rais ili waendelee kuwa
“Majembe” katika Wizara hiyo.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe kutoka nchi nzima ambao watahakikisha nchi imefika hatua ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 kulinganana na malengo iliyojiwekea katika mpango mkakati wake.








0 comments:
Post a Comment