Tuesday, April 1, 2014

Video: Tizama official video trailer ya wimbo ulioimbwa na wasanii zaidi ya 19 Africa akiwemo Diamond

Zaidi ya wasanii watano kati ya wale 19 waliojumuika kutengeneza wimbo na video ya wimbo "Cocoa na Chocolate" kwa ajili ya kuhamasisha kilimo kwa vijana na kuwa kiimo kinalipa, wamekutana Lagos nchini Nigeria kwa ajili ya uzinduzi wa video hiyo, huku watagazaji mbali mbali kutoka mchi mbalimbali nao wakihudhuria uzinduzi huo akiwemo Fetty, Fettylicious Fe;eh.
Zaidi ya wasanii 19 kutoka katika nchi mbali mbali Africa wakiwemo Diamond (Tanzania) D'Bhanji na Femi Kuti (Nigeria), Fally Ipupa (DRC) na wengineo walikutana nchni south Africa na kutengenea wimbo wa pamoja unaohamasisha vijana kujihusisha na maswala ya kilimo na kuwaambia vijana wa kiafrica kuwa maisha yao ya baadae yako chini ya miguu yao wenyewe na katika mikono yao wenyewe.
Video hiyo imeshakamilika na alhamis ya wiki hii itaonyeshwa katika TV station Mbali mbali Ikiwemo Clouds TV kutoka Tanzania.
Tizama trailer ya video hiyo iliyotoka leo hii
Source: Dj Fetty Blog

0 comments:

Post a Comment