Tuesday, April 22, 2014

Moyes afukuzwa rasmi Mancherster United

Kocha na meneja wa klabu ya Manchester United David Moyes ametimuliwa rasmi. 

Moyes amefutwa kazi baada ya kuifundisha klabu hiyo klabu hiyo kwa miezi kumi tu.
Klabu hiyo hapo awali ilikuwa imekataa kuzungumzia udaku wa magezti kuwa Moyes atafutwa kazi kabla ya msimu kumalizika.
Moyes, mwenye umri wa miaka 50, aliteuliwa na Ferguson kumrithi alipostaafu mwaka jana baada ya kuwa na klabu hiyo kwa miaka 26.
Taarifa kutoka kwa klabu hiyo imemshukuru Moyes kwa bidii, uaminifu na hekima aliyoonyesha kocha huyo akiwa mkufunzi wa Manchester United.

Huku zikiwa zimesalia mechi nne pekee msimu wa ligi kukamilika Mancheseter united inashikilia nafasi ya saba kwenye jedwali la msimamo wa ligi hiyo alama ishirini na tatu nyuma ya viongozi Liverpool.
Klabu hiyo imeshindwa kufuzu kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa ulaya kwa mara ya kwanza katika kipindi cha takriban miaka ishirini.

0 comments:

Post a Comment