
Mwanamke anayeshikilia cheo cha juu zaidi katika
kampuni ya Facebook, amewataka wanawake kuchukua hatua za kubuni
mazingira ya usawa kote duniani.
Sheryl Sandberg, Ofisa mkuu wa mipango katika
Facebook, amesema kuwa wanawake, wanapaswa kushikilia nafasi muhimu
katika biashara.Sandberg ni mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa huo katika kampuni hiyo tangu mwaka 2012.
Mwaka jana aliandika kitabu kwa jina 'Lean In' ambacho kinawashauri wanawake kuhusu wanavyoweza kupiga hatua katika nafasi zao za kazi.
"ni muhimu sana kwamba wanawake ambao ni nusu ya idadi ya watu wote, waanze kushikilia vyeo katika meza za maamuzi , lakini bado hatujafika hapo, '' alisema .
Alisema kuwa wanawake wanaweza kuwa viongozi muhimu sana katika biashara,serikali ni pamoja na kuwa wajasiri amali
Akizungumzia baadhi ya changamoto zinazokumba Facebook, Sandberg alisema kuwa dunia inashuhudia mageuzi makubwa ya kiteknolojia ambayo yanahusisha simu ya rununu na Facebook ipo katikati ya mageuzi hayo
0 comments:
Post a Comment