NI MWANADADA
aneyejulikana kwa jina la Anastasiya Shpagina ambaye ni mmoja tu kati
ya wasichana wengi kutoka Ukaraine ambao wamejibadilisha miili yao kwa
kufanyiwa plastic surgery na kuwa katika miundo ya midoli na wenyewe
hujiita 'Barbie'….
...Usijedhani
ni mdoli tu na si mtu kweli, amini usiamini dunia hii haiishi
vijimambo, huyu ni mtu kweli na si feki ambaye ameamua kujibadilisha na
kuonekana hivi...
Anastasiya alifanyiwa upasuaji na kupunguzwa kiuno chake, hali nyama…
cha
kushangaza mwanadada huyu anataka kufanyiwa upasuaji zaidi kukipunguza
zaidi kiuno chake na kuyafanya macho yake yaonekane makubwa zaidi ya
yanavyoonekana kwa sasa,
Haya yote yanatokea akiwa na umri wa miaka 19
Akiwa na doll mwingine aitwaye Valeria Lukyanova (kushoto)
Daaaaaah! wangekuwa dada zako ungefanyaje sasa….!!!!???
Ndo Basi tena..
Huyu ni Venus Angelic kutoka London….
Wanadada hawa wan a ukurasa wao wa Facebook uitwao HUMAN DOLLS.... Waweza pia utazama na kushuhudia yote haya.
Ukiacha
na upasuaji huo waliofanyiwa, wanadada hawa hutumia muda mwingi kukaa
katika vioo vyao kufanya make up kwaajili ya kutengeneza macho yao yawe
na muonekano wa midoli hiyo maarufu kama 'Barbie' Barbie Dolls, kwa
mfano Anastasiya yeye hutumia zaidi ya dk 30 kwa jicho moja, kulichora
na kulipaka vitu anavyovijua yeye ili apate muonekano huo wa mdoli.
Ukitembelea
katika vyanzo mbalimbali utagundua kuwa watu wengi wanashauku ya kujua
hali za afya za akina dada hawa ambao wameona wajibadili maumbo yao ya
kawaida na kuwa midoli watt.
Ambapo
dada mmoja ajulikanaye kama Valeria anasema anatarajia kujibadili kwa
kupigwa na mionzi ili awe anachajiwa kama vile unavyochaji simu na
kuitumia badala ya kula kama kawaida kwani anaona kula ni shida sana…..
Anamaanisha anataka kuwa mdoli kabisaaaa. Daaah sasa huyu ndio shida
kabisaa.
Hapa chini ni Anastasiya Shpagina akifanya mahojiano na kituo kimoja nchini Ukraine. Hebu nawe shuhudia maajabu haya!!!
















0 comments:
Post a Comment