Kikundi cha Sanaa cha Tasuba wakionesha moja ya ngoma za Asili wakati wa moja ya Onesho lao.
Kikundi cha Sarakasi kikionesha umahiri wa mchezo huo katika onesho lake
Wasanii wa Mchezo wa Kuingizwa unaofanywa na Walimu ukiwa na hisia kali wakiwa jukwaani.
Kikundi cha Wasanii kutoka Nchini Norway wakiwa jukwaani kutowa burudani.
Na Andrew Chale, Bagamoyo
TAMASHA la Kimataifa la Sanaa na
Utamaduni Bagamoyo ambalo kwa mwaka huu (2014) litakuwa la 33, ambapo
linatarajia kulindima kwa siku saba, kuanzia Septemba 22 hadi 28, kwenye
viunga vya Chuo cha Sanaa Bagamoyo.
Tamasha hilo la 33, mwaka huu, lenye
kauli mbiu, “Sanaa na Utamaduni katika kukuza Utalii”, limekuwa msaada
mkubwa kwa wasanii na vikundi mbali mbali kujitangaza kitaifa na
kimataifa pamoja na kutoa fursa za kibishara katika kipindi chote cha
tamasha.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tamasha hilo,
Abraham Bafadhil ‘Bura’, alieleza kuwa, tayari mipango na maandalizi
ya tamasha hilo yanaendelea katika kufikia malengo huku akiwaomba wadau
kujitoakeza na kudhamini tamasha hilo.
“Milango ipo wazi hivyo, kwa wadhamini
kujitokeza na kuchangamkia fursa hii hadimu, kwani tamasha hili ni
kongwe katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki na Afrika kwa ujumla”
alisema Bura.
Na kuongeza kuwa, tamasha hilo lenye
mvuto wa kipekee ndani na nje ya Tanzania, limekuwa likipata umaarufu
mkubwa kila mwaka kutokana na idadi kubwa ya watazamji wa ndani na wale
wa kutoka Mataifa mbali mbali duniani.
Kwa upande wake, Katibu wa tamasha hilo,
Benjamini Mahimbali alieleza kuwa, tamasha hilo limekuwa na mafanikio
ikiwemo ongezeko kubwa la watazamaji na vikundi vinavyoomba kufanya
maonyesho.
“Idadi ya watazamaji na imekuwa
ikiongezeka kila mwaka, huku kwa mwaka jana tulikuwa na wastani wa
watazamaji elfu nne mia saba kwa siku (4,700), ikiwemo wa rika zote.”
Alisema Ben.
Na kuongeza kuwa, wanatarajia ongezeko
hilo kuwa kubwa zaidi kutokana na maboresho na mipango mbali mbali
inayotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Katika tamasha hilo maonyesho mbali mbali
yanatarajiwa kuonyeshwa ikiwemo; Muziki wa aina tofauti, ngoma,
maigizo, sarakasi, mazingaombwe na maonyesho kemkem ya sanaa na
utamaduni wa Mtanzania na ya Mataifa mengine duniani.
Kwa upande wa fomu za kushiriki tamasha
hilo ambalo kwa mwaka huu wanatarajia kupokea vikundi zaidi ya 40,
zinatarajiwa kutolewa kwenye ofisi za Chuo hicho pamoja na tovuti ya
chuo (www.tasuba.ac.tz)
Au Kwa mawasiliano na maulizo juu ya ushiriki na udhamini waweza kufika Chuo cha Sanaa Bagamoyo (Tasuba) au kupitia namba;














0 comments:
Post a Comment