Akizungumza
katika Kikao cha kuwasilisha ripoti ya tathmini ya Tamasha la Krismasi
iliyofanyika jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Basata, Ofisa Sanaa wa
Basata, Rajabu Zubwa alipongeza licha ya kwamba imekumbana na changamoto
ikiwa pamoja na kulipeleka mkoa wa Tanga ambao una idadi kubwa ya
waislamu ni wengi.
Zubwa
pamoja na kupongeza alitoa mapendekezo yatakayopunguza gharama katika
tamasha hilo na ili kufanikisha gharama ambazo zitawafikia walengwa
ambao ni wenye uhitaji maalum, Kamati hiyo inatakiwa kupunguza waimbaji
kutoka nje kwa kuwa viingilio ni vidogo. “Mnapoandaa tamasha jaribuni
kutulia sehemu moja kwa ajili ya kukwepa hasara pia punguzeni idadi ya
watu ni kubwa, gharama haiwezi kurudi,” alisema Zubwa.
Naye
Ofisa Sanaa Mkuu, Philemon Mwasanga alipongeza Msama kuandaa tamasha
hilo na kueleza lilikuwa zuri na aliishauri Kamati kuwa makini na
ualikaji wa waimbaji kutoka nje ya nchi kwa kuwa wengi wamekuwa
wakifanya kinyume na maadili ya ufikishaji wa Neno la Mungu kwa njia
ya uimbaji.
Alisema
waimbaji wengi wa sasa wamemuweka Yesu nyuma hawana tofauti na
wanamuziki wa Bongo Fleva huku akitaka ziwekwe sheria za tamasha kwa
waimbaji hao zitakazodhibiti mambo mbalimbali ikiwemo mavazi,
nidhamu na mengineyo.
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Abihudi Mang’era
alisema wamekumbana na changamoto nyingi ikiwa pamoja na kutopata
wahudhuriaji wengi katika mkoa wa Tanga.
Mang’era
alisema changamoto nyingine ni viingilio vidogo hasa ukizingatia hakuna
wadhamini kabisa na alitumia fursa hiyo kuwaomba Basata kuliona hilo na
kuwasaidia katika matamasha yake yajayo.
0 comments:
Post a Comment