Mwenyekiti wa
CCM Taifa Dk.Jakaya Kikwete akizungumza na wajumbe wa NEC wakati wa
ufunguzi wa kikao cha NEC ambacho kinaendelea leo mjini Dodoma , kushoto
ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk. Ali Mohamed Shein na kulia
ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Wajumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wakipitia magazeti yalotoka leo Februari
16,2014 kabla ya kuanza kwa kikao cha NEC mjini Dodoma ambacho leo
kinategemewa kumalizika.
Katibu wa NEC
Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akizungumza na
Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro Ndugu Steven Kazidi kabla ya kuanza
kwa kikao cha NEC mjini Dodoma leo Februari 16,2014.
Naibu Katibu
Mkuu wa CCM(Bara) Ndugu Mwigulu Nchemba akijadiliana jambo na wajumbe wa
NEC Ndugu Said Nkumba na Jestina Mhagama kabla ya kikao cha NEC
akijaanza mjini Dodoma.
Pichani ni
Wajumbe wa NEC kutoka Zanzibar Dk.Maua Daftari na Asia Sharif wakati wa
kikao cha NEC kinachoendelea mjini Dodoma ambapo moja ya mambo
yanayojadiliwa ni Rasimu ya Katiba.
Wajumbe wa NEC
kutoka Kusini Unguja Ndugu Ramadhani Abdala Shabani na Ndugu Mussa
Makame maarufu kwa jina la Dere wakizungumza nje ya ukumbi wa NEC kabla
ya kikao hakijaanza.
Profesa Mark
Mwandosya akizungumza na Godfrey Zambi nje ya ukumbi wa NEC kabla ya
kuanza kwa kikao cha NEC ambacho kinatarajiwa kumalizika leo mjini
Dodoma.
0 comments:
Post a Comment