Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi
(kushoto) akifungua warsha ya mafunzo ya mfumo wa biashara ya hewa
mkaa, na athari za mabadiliko ya tabia nchi,mjini Bagamoyo leo.(kulia ni
Injinia. Ladslaus Kyaruzi Afisa Mazingira Mwandamizi kutoka Ofisi ya
makamu wa Rais.
Baadhi ya washiriki, wa warsha ya mafunzo ya mfumo wa biashara ya hewa mkaa mjini bagamoyo leo.
Picha ya washirki wa warsha ya mafunzo ya mfumo wa Biashara ya hewa mkaa mjini Bagamoyo leo.
======= ======== ==========
NA EVELYN MKOKOI
Kuongezeka
kwa kina cha bahari, kuongezeka kwa gesi joto, kupungua kwa barafu
hususan katika mlima Kilimanjaro na mabadiliko ya mfumo ya mvua,
Imeelezwa kuwa ni changamoto kubwa zitokanazo na athari za mabadiliko ya
tabia nchi nchini.
Hayo
yameelezwa leo na Mkurugenzi msaidizi kutoka Ofisi ya Makamo wa Rais
Mazingira, Bw Richard Muyungi katika ufunguzi wa warsha ya mafunzo wa
biashara ya hewa ukaa, mjini Bagamoyo iliyohusisha wataalam wa masuala
ya mazingira kutoka katika sekta mtambuka nchini.
Bw.
Muyungi ameeleza kuwa, Shughuli za kibinadamu hasa katika nchi
zilizoendela kama vile za uzalishaji viwandani zimekuwa zikichangia kwa
kiasi kikubwa katika kuleta athari za mabadiliko ya tabia nchi..na hii
inatokana na kuachiwa kwa kiasi kikubwa cha hewa ya ukaa kutoka
viwandani kwenda angani, ambapo ongezeko la joto ni kichocheo kikubwa
cha athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.
Bw.
Muyungi aliongeza kuwa uzalishaji wa gasijoto katika maeneo mengine,
kama misitu, kilimo, joto, usafirishaji, majengo na methane huzalishwa
kwa kiasi kikubwa katika nchi zilizoendelea na uleta athari za
mabadiliko ya tabia nchi.
”Katika
nchi zinazoendelea umaskini ndo unasababisha ukataji ovyo wa misitu na
kuiuza kwa bei rahisi, aidha matumizi mabaya ya mbolea katika sekta ya
kilimo huchangia pia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa gesi joto.”
Alisisitiza
Tanzania ni nchi mojawapo iliyoridhia mkataba wa kimataifa wa
mabadiliko ya tabia nchi tangu mwaka 1996 na itifaki ya Kyoto ya mwaka
2002 ukiwa na lengo kubwa la kupunguza uzalishaji wa gesijoto.








0 comments:
Post a Comment