Tuesday, December 10, 2013

Maziko ya Paul Walker kuhudhuriwa na wanafamilia tu

Mazishi ya  Paul Walker yanatarijiwa kuwa ya binafsi ... ambapo imeelezwa itakuwa ni kwa ajili ya familia tu, pamoja na baadhi ya crew ya fast & Farious.

Vyanzo vya karibu vyenye uhusinano na familia ya Walker viliiambia TMZ kuwa wasiwasi wao mkubwa ni binti wa Walker mwenye umri wa miaka 15  Meadow, ambaye kwa kwa sasa yupo katika wakati mgumu, hivyo familia hiyo hawataki kundi kubwa la watu kuwa jirani na binti huyo, kwa sababu anahitaji kujisikia vizuri na kuondokana na huzuni aliyonayo.
Hivyo mazishi ya Walker yatakuwa na mwaliko maalumu kwa watu watakaopewa, na pia inaelezwa kuwa baada ya mazishi kutakuwa na kumbukumbu itakayofanyika lakini pia itakuwa ni kwa mwaliko.

0 comments:

Post a Comment