Monday, December 16, 2013

Dk Mengi akana kumiliki eneo kubwa la madini

MWENYEKITI Mtendaji wa Kampuni za IPP Limited, Dk Reginald Mengi amekanusha kumiliki eneo kubwa la migodi. Akizungumza jana, Mengi alisema eneo analomiliki kwa ubia na Watanzania wenzake ni mgodi mmoja wa uchimbaji wa madini ya tanzanite lisilofikia hata kilometa moja ya mraba.
“Desemba 8 mwaka huu, alipokuwa anajibu swali la Tundu Lissu kuhusu ni nani anamiliki migodi ya Tanzania, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo (Sospeter) alitoa takwimu za kunihusu ambazo si sahihi.
“Ukweli ni kwamba mimi namiliki kwa ubia na Watanzania wenzangu mgodi mmoja wa uchimbaji wa madini ya tanzanite wenye eneo lisilofikia hata kilomita moja ya mraba na siyo Dar es Salaam 3 kama alivyosema.”
Dk Mengi alisema Waziri Muhongo amekuwa akitoa taarifa kama hizo mara kadhaa ikiwemo pia wakati wa Mdahalo wa rasilimali uliofanyika Desemba 8, mwaka huu katika Ukumbi wa Nkrumah, Dar es Salaam ambapo Profesa Muhongo alitoa takwimu zinazoonesha Dk Mengi anashika nafasi ya tatu ya Watanzania wanaomiliki maeneo makubwa ya uwekezaji.
Profesa Muhongo alisema, Mengi anamiliki eneo ambalo ukubwa wake ni mara tatu ya ukubwa wa Dar es Salaam na kuwa hana cha maana anachonufaisha Watanzania na badala yake kujinufaisha mwenyewe.
SOMA ZAIDI: HABARILEO ONLINE

0 comments:

Post a Comment