KATIKA
moja ya mambo yaliyojitokeza katika mgogoro wa uongozi wa Chadema, ni tathmini
ya nguvu za aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Kabwe Zitto dhidi ya kinachoitwa
udhaifu wa Mwenyekiti wa sasa wa chama hicho, Freeman Mbowe na uongozi wake.
Tathmini
hiyo ambayo aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Dk Kitila Mkumbo jana
ameiita kuwa ni siri iliyowekwa wazi kwa makosa ya kijinga, imeeleza namna
kiongozi huyo alivyoandaa mkakati wa kumuondoa Mbowe madarakani kidemokrasia,
kupitia nguvu za Zitto.
“Nani
tumuunge mkono kuchukua nafasi ya Mkuu (Mbowe). Utangulizi huo (udhaifu wa
Mbowe) unaoonesha kinagaubaga kwamba tunahitaji mabadiliko na hatua iliyofuata
ilikuwa ni kuangalia nani anaweza kuleta mabadiliko tunayohitaji.
“Ni
vema ikazingatiwa kwamba mtu ambaye tungemuunga mkono lazima awe mwenye uwezo
mkubwa kuliko tunayetaka kumtoa (Mbowe). Awe ana sifa za kiuongozi na zaidi
sana awe na uwezo wa kupambana na mkuu aliyeko.
“Katika
kuchunguza ndani ya taasisi (Chadema), tuliridhika kwamba Mtendaji Mkuu
Msaidizi (Naibu Katibu Mkuu, Zitto), ana sifa zote tulizozitaja hapo juu ingawa
kila mwanadamu ana udhaifu wake.
“Ni
dhahiri pia kwamba udhaifu wa Mtendaji Mkuu Msaidizi unarekebika kuliko wa mkuu
aliyepo,” umeeleza mkakati ambao Dk Mkumbo amekiri kuuandaa na kusisitiza
hajutii kazi hiyo aliyoiita ni ya matamanio ya mabadiliko ndani ya Chadema.
“Nasisitiza
tena kwamba siamini hata kidogo kwamba matamanio ya mabadiliko ya
uongozi
ndani ya chama, na kuandaa mikakati ya kufikia matamanio hayo kwa njia za
kidemokrasia ni uhaini,” alisisitiza Dk Mkumbo alipokutana na waandishi wa
habari Dar es Salaam kukiri kupanga kumuondoa Mbowe na uongozi wake madarakani.
*Udhaifu
wa Mkuu
SOMA ZAIDI: HABARILEO ONLINE








0 comments:
Post a Comment