Na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania
JAJI wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe.Dr.
Stephen Bwana anatarajia kuapishwa kesho (Alhamisi) kuwa Jaji wa Mahakama ya
Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) ya nchini Cambodia.
Uapisho
huo unafuatia baada ya kuteuliwa kwake na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe.
Ban. Ki Moon kwa kushauriana na Mfalme wa Cambodia, Mtukufu Norodom Sihamoni
mnamo tarehe. 09.05.2012.
Mhe. Dr. Bwana ataongozwa kiapo na Rais
wa Mahakama hiyo aliyeko nchini Cambodia kupitia Video katika Ofisi za WFP
zilizopo Upanga jijini Dar es Salaam kuanzia 02:45 asubuhi.
Kabla ya Uteuzi huo Mhe. Dr. Bwana
ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani (T) aliwahi kushika nafasi mbalimbali kama
Jaji wa Mahakama Kuu, Seychelles, 1994-1999, Jaji wa Mahakama ya Rufaa ya
Seychelles 2004-2009, pia Kaimu Rais wa Mahakama hiyo ya Rufani kuanzia mwaka
2006-2008.
Mbali na kushika nyadhifa hizo, Dr. Bwana
pia aliwahi kuwa, Mshauri wa Benki ya Dunia kuhusu Uboreshaji wa Shughuli za
Mahakama, Afrika (2003-2008), Msajili, Mahakama ya Rufani (T), 1989-1994,
Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania 1989 na Hakimu Mkazi 1974.








0 comments:
Post a Comment