
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,
Mkurugenzi Mtendaji wa TDL, David Mgwassa, alisema ana uhakika kinywaji hicho
kitapendwa na wengi, kwani ni cha Kitanzania na kimezingatia ubora wa kiwango
cha Kimataifa katika uzalishaji wake.
Mgwassa aliwataka Watanzania
kujivunia kinywaji hicho na kusema TDL ikiwa ni kampuni ya kizalendo itaendelea
kuhakikisha inazidi kuitangaza Tanzania kwa kuzalisha bidhaa bora zinazopendwa
na wengi ndani na nje ya nchi.
“Kwetu sisi TDL tunajivunia kuzindua
rasmi kinywaji cha Zanzi Cream Liqueur kwani kinazalishwa na Watanzania
na kimebuniwa na wazalendo wa nchi hii. Huu sasa ni wakati wa kutembea kifua
mbele kujivunia kinywaji hiki na naamini kitavutia wengi kutokana na jinsi
kilivyotengenezwa na kikiwa na ubora usio na shaka.”
Mgwassa alisema, nia ya kuzalisha
kinywaji cha Zanzi Cream Liquer ni baada ya kuona kuna vinywaji vingi
vya aina hiyo vikiingizwa nchini kutoka nje, hivyo TDL ikataka kuzalisha bidhaa
bora zaidi na ya kipekee hapa duniani.
Naye Meneja Masoko Taifa wa TDL,
Joseph Chibehe, alisema kinywaji hicho kitapatikana katika chupa zenye ujazo wa
mililita 750 na pakiti zenye ujazo wa mililita 100, huku kikiuzwa kwa bei
ambayo watu wengi wataimudu.
0 comments:
Post a Comment