Thursday, December 27, 2012

R.O.M.A 2030 INTRO

SONG 2030
PRODUCTION TONGWE RECORDS
PRODUCER J RIDER + YUDDI
2030
Ni jibu la mathematics, ambapo kule tulikuwa tunatafuta thamani ya "X"
sasa tumepata X=2030, falsafa yake ni kuwa ni wimbo unaomuhusu mtoto aliyezaliwa
mwaka huu ambao wimbo umetoka yaani 2012, na kwakuwa mapinduzi na changez
huanzia nyumbani, basi nilifanikiwa kupata mtoto wa kiume mwaka huu october 4th
nikamuita IVAN(means GIFT FROM GOD).
Kwakuwa miaka ya mtanzania kufikisha umri wa utu uzima ni
miaka 18, basi aliyezaliwa leo 2012 hadi afikishe umri huo wa miaka 18 basi
itakuwa ni 2030.
(Mathematically 2012 + 18 =2030) hiyo ndiyo falsafa yake.
So ni wimbo ambao ni kama mtoto mchanga IVAN, na wote waliozaliwa kipindi hiki
cha mwaka ambao wimbo umetoka, na yaliyoongelewa ndani ya wimbo na ndani ya album
itakayokuwemo nyimbo hii, ni maneno ambayo yatamjenga mtoto huyu aliyezaliwa sasa
katika misingi bora, tukisaidiana kwa pamoja sisi tuliokwisha liona jua, kuwalea hawa
waliozaliwa sasa katika misingi hiyo bora ili wakifikisha umri huo wa miaka 18
wawe ni miongoni mwa vijana ambao watakuja kuleta changes katika jamii na taifa kwa ujumla
(positive impacts). Katika misingi mizuri miaka hiyo ya usoni kuanzia mwaka huo wa 2030!!
Haya yatawezekana kama tutawalea katika malezi mazuri kiimani,kitaaluma,
kiafya, kitamaduni, kiamani, kiupendo, kibusara na maadili mema na yote
tuliyoagizwa katika wimbo huu na album kwa ujumla!!
Kwa hiyo hata sisi wazazi/walezi/viongozi/vijana/wazeee na jamii yote kwa ujumla inatuhusu hii nyimbo, kwani tukiungana kwa pamoja na kuyaishi haya basi nina maono
ya kuwa mwaka 2030 tutakuwa tumeshafanya changez kubwa kwa taifa letu au utakuwa ndio mwanzo mzuri wa kuleta mapinduzi chanya hapa nchini,na jamii kiujumla.
(SACRIFICE FOR YOUR SONS n DAUGHTERS, ILI WAJE KUISHI VEMA)
wimbo huu umezaliwa leo na tuubariki maneno yake yaishi kwa miaka hiyo
na zaidi ili kunako 2030 tuone na tujivunie matunda ya mtoto huyu
hapo akiwa na miaka 18!!
THANX GOD FOR HAVIN I.V.A.N nipe busara, akili,
na hekima nimlee katika misingi uliyotuagiza!! nanyi mkayaishi kayo
niliyowatuma!!! HALELUYAH!!
R.O.M.A Z BACK VRUUM TONGWE RECO RDS BEEIB... u know TANGA z ma hood!!!


 

0 comments:

Post a Comment