Thursday, October 11, 2012

SHINDANO LA MFALME WA ‘KURAP’ KUANZA RASMI JUMAPILI HII DAR LIVE

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).

Mratibu wa shindano hilo, Luqman Maloto akinena jambo kwenye mkutano huo

SHINDANO la kumtafuta Mfalme wa Kurap Bongo lililoandaliwa na Ukumbi wa Dar Live, litaanza Jumapili hii katika ukumbi huo uliopo Mbagala, kikini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Atriums iliyopo Sinza Afrika Sana, jijini Dar, Meneja Mkuu wa kampuni ya Global Publishers Ltd ambao ndio wamiliki wa ukumbi huo, Abdallah Mrisho, amesema mshindi atazawadiwa gari la kifahari ambalo litatangazwa hivi karibuni.
Kuanziakesho, vijajna wajitokeze pale Dar Livekwa wingi ili kushiriki. Jumapili ya wiki ijayo ndiyo watapata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao, na mchakato mzima wa kumtafuta mshindi ndiyo utakuwa umeanza rasmi,” alisema Abdallah.
Aidha, mratibu wa shindano hilo, Luqman Maloto, amesema watu wajitokeze kwa  wingi kwani hakuna ‘longolongo’ na majaji watakuwa watu wenye heshima kubwa kwenye gemu ya muziki Bongo pamoja na wananchi watakaokuwa wakihudhuria Dar Live.
                                                                                                                            (PICHA/HABARI: ERICK EVARIST/GPL)




0 comments:

Post a Comment