
MSANII
wa muziki wa kizazi kipya, Ben
Pol, amesema kuwa kutokana na ngoma yake ya ‘Pete’, kufanya
vizuri sasa anatarajia kutengeneza video ya ngoma hiyo ambapo kazi hiyo
itasimamiwa na timu ya Ogopa
Deejays kutoka Nairobi Kenya ambao watatua bongo kupiga kazi......>>>
Alisema
kuwa video hiyo gharama yake itakuwa si chini ya milioni 6 kwani ameamua
kufanya hivyo ili kutengeneza kazi yenye kiwango na si zile ambazo watu
wamekuwa wakizoea kuziona, ambapo anaamini kazi hii itamuwezesha kufanya vizuri
zaidi katika muziki wake.
Hata
hivyo msanii huyo aliongeza kuwa kufanya kazi na Ogopa ni kufungua
njia ya kuvuka mipaka na kuingia Kenya kwani wapo wasanii kibao wa nchini
humo anaotaka kufanya nao kazi siku za usoni.
0 comments:
Post a Comment