Wednesday, October 17, 2012

Nasema Nao Rmx yamuingiza Ney wa Mitego matatani

 
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchinim Ney wa Mitego, yupo kwenye hatihati ya kufungiwa na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) baada ya kuachia remix ya wimbo wake wa Nasema Nao uliojaa matusi na maneno makali dhidi ya wasanii wenzake na watu mbalimbali.
Kwa mujibu wa afisa mmoja wa Basata aliyeomba hifadhi ya jina lake kwani si msemaji rasmi, katika wimbo huo ulioanza kusikika mwishoni mwa wiki iliyopita, Ney wa Mitego ametumia lugha ya matusi na maneno yasiyo ya kistaarabu, huku akiwataja kwa majina watu aliowalenga, jambo ambalo ni kinyume na sheria za baraza hilo.
Baada ya kupata nyepesi hizo kutoka Basata, Showbiz ilimtafuta Ney wa Mitego ambaye alisema kuwa wimbo huo wa Nasema Nao Remix umevujishwa na watu asiowatambua bila idhini yake lakini akaeleza hajapokea taarifa yoyote kutoka Basata juu ya kufungiwa.

GPL
 

0 comments:

Post a Comment