Friday, October 12, 2012

MNAZALETI AJIPANGA KUACHIA ALBAM

 


BAADA ya kufanya vizuri na ngoma yake ya ‘Chukua Time’ msanii Suma Mnazaleti, amesema kuwa anafikilia kuachia albamu baada ya ngoma yake inayokuja kwenda sokoni, ingawa awali kabisa hakufikiria kama anaweza kuachia albamu kwani alipaga kutoa ngoma moja moja tu.

Msanii huyo alidai kuwa ngoma hiyo inayokuja atafanya na Rich Mavoko akidai ndiye msanii ambaye kwa sasa anaona anaweza kusimama katika ngoma yake ingawa bado ngoma hiyo mpya hajaipa jina.


Suma alisema kuwa wazo la kutoa albamu limekuja baada ya kuona kuwa ana kazi nyingi ambazo tayari amesha zirekodi na njia nzuri ya mashabiki wake kuzisikia ni kupitia albamu.

“Awali kabisa nilikuwa narekodi ngoma naweka ndani na siyo kwamba ni mbaya hapana ni ngoma kali sana, lakini nashindwa kuzitoa kwa sababu kadri siku zinavyokwenda napata wazo lingine la ngoma kali, kitu ambacho nimefikiria sasa ni kuzitoa kwa njia ya albamu tu ili mashabiki wangu waweze kuzisikiliza,” alisema.

0 comments:

Post a Comment