Monday, October 22, 2012

KIBAHA are you readyyyyyy, NISHIKE MKONO Tour inaanzia hapo tarehe 26 mwezi huu

 
PROFESSOR JAY FOUNDATION Kwa kushirikiana na 100.5 TIMES FM inakuletea ziara ya kitongoji kwa kitongoji Tuliyoipa jina la NISHIKE MKONO TOUR, ikiwa na nia ya kusaidia sehemu husika kwenye sekta ya ELIMU NA AFYA, Na kwa kuanzia tunaanza ijumaa ijayo Tar 26 pale KIBAHA CONTENER Na tar 27 CHEM CHEM - MLANDIZI, Wasanii kibao wamekubali kushirikiana nasi kwenye hili suala la kijamii Kwa njia moja ama n yingine, kama vile JUMA NATURE, SUGU, AY, FA, AFANDE SELE, MADEE, NAY WA MITEGO, LINEX,BLACK RHYNO, BARNABA,MATONYA, SQUEEZER, MBATIZAJI na wengine kibao Na pia wengine wengi tunaendelea kuwajuza kuhusu hii dhamira yetu, yoyote atakayependa kushirikiana nasi pia anakaribishwa sana pia awasialiane nasi tafadhali kwa sababu hili suala ni la wote na sio letu pekee, tucheki kwenye email yetu ya professorjayfoundation@gmail.com, MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRICA!!

0 comments:

Post a Comment