Friday, October 19, 2012

DAH! BINADAMU TUNATOKA MBALI SANA, HEBU TAZAMA HUKU NILIPOANZIA MUZIKI - DIAMOND

Daah! Maisha ni safari ndefu sana ndugu zangu na hakuna anae jua wapi anaelekea wala aliyezaliwa anajua chochote,siku zote mwanzo huwa mgumu sana ukiongeza na maneno ya watu ya kukukatisha tamaa basi ndio unazidi kuyaona Maisha magumu na kukata tamaa na kujiona huwezi kabisaaaa!... Mimi wakati naanza muziki nilikutana na mambo mengi sana ya kukatisha tamaa lakini siku zote sikuchoka kumuomba Mwenyezi Mungu anisaidie na kuzidisha juhudi kila dakika..... 
Naitumia nafasii hii pia kuongea na wasanii wachanga wanaochipukia kwenye sanaa ya muziki wasikate tamaa na hizi ni kama nguzo zinazoweza kukufanya angalau kupiga hatua.....Kwanza kabisa ni Maombi,Uvumilivu,Juhudi,Ubunifu na Heshima inahitajika sana.....Ukiangalia Video yangu ya Toka mwanzo na hiyo ya Mawazo niwazi kabisa utajionea utofauti mkubwa sana na utakubaliana na mimi ama kweli
 MAISHA NI SAFARI NDEFU SANA.


                                                 

0 comments:

Post a Comment