Edge Entertainment Co Ltd imeandaa tamasha kubwa la muziki wa
dansi linalojulikana kwa jina la Tanzania Live Music Festival litalofanyika kwa
muda wa siku mbili kuanzia Septemba 28 na 29, katika viwanja vya Leaders Club kuanzia
saa 10:00 alasiri na kuendelea.
Tamasha hili lina lengo la kukuza muziki wa dansi nchini
Tanzania, kukusanya fedha kwa ajili ya kukisaidia Chama cha Muziki wa Dansi
(chamudata) kiweze kujiendesha kwa ufanisi. Kuchangia mfuko wa sanaa ulio chini
ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
Tamasha hili litajumuisha bendi mbalimbali za muziki
wa dansi nchini na litakuwa likifanyika kila mwaka, na tunatarajia kwa miaka
ijayo kukutanisha bendi mbalimbali nchini na kualika bendi au wanamuziki
wakubwa kuja kushiriki toka nje ya Tanzania.Katika kufanikisha tamasha tumemchagua Jackline Wolper kuwa Balozi wa tamasha hili kwa mwaka 2012.
Siku moja kabla ya tamasha 27/9/2012 kutakuwa na mafunzo ya siku moja kwa wanamuziki kuhusu hati miliki yatakayotolewa na COSOTA.








0 comments:
Post a Comment