MSANII wa filamu ambaye ameamua kuigia upande wa pili wa muziki, Snura,
ameuambia mtandao wa DarTalk, kuwa haitaji
kuonekana anafanya show bali malengo yake ni kuleta mapinduzi katika
muziki huo na suala nzima la kulitawala stage ili azidi kujiweka tofauti
na wengine.
Msanii huyo alisema wasanii wengi wa Tanzania ni wa wavivu kwenye kutawala stage kwani mara zote huwa wanasimama sehemu moja kutokana na uvivu huku hata kucheza wanashindwa kutokana kujiona na wengine wanawatumia sana wacheza show wao.
Msanii huyo alidai kuwa ameamua kufanya muziki basi hawezi kutoa ngoma nyepesi nyepesi kwani anamini watanzania wanataka kuona nini anachokifanya, huku mapingo yake katika muziki huo ni kuonesha kazi kama wasanii wa nje ambao wanafanya muziki kwa kujituma na si kujionesha kama baadhi wa hapa bongo.
“Tazama wasanii wengi wa bongo kwenye suala la kucheza wao ni wavivu, hivyo kwa upande wanu sihitaji kuwa kama wao na ndiyo maana nafanya mazoezi ya kutosha kwani naelewa muziki unataka nini na watu wangu wanataka nini kwa wakati gani,” alisema.
Aliongeza “kwa wale wabaya wangu hata kama wakizidi kuniombea mabaya hawawezi kunipata kwani ‘dua la kuku halimpati mwewe’ na kwa njia hiyo nitazidi kuchanua na kufika mbali zaidi.”

0 comments:
Post a Comment