Monday, September 3, 2012

“SIKUJUA KAMA ‘JAFFARAI’ NI KAKA YANGU MIAKA YOTE ” – Z-ANTO…!!




MSANII wa muziki wa kizazi kipya bongo Z-anto, amesema kuwa hakuna kitu alichokuwa anakijua kuhusiana na msanii mwezake Jaffarai, lakini msiba uliotokea nyumbani kwao Mtwara ndiyo uliowakutanisha na hadi wao kujuana kuwa wao ni ndugu wa damu , na kuwa Jaffarai ni kaka yake.

Z-anto alisema awali alienda kusalimia nyumbani kwao Mtwara na alipofika huko, ndipo alipata taarifa kuwa Jaffarai katoka hapo kwao muda si mrefu, na hapo ndipo alipojiuliza maswali mengi juu ya msanii huyo.
Aliendelea kusema kuwa hakuendelea kuhoji na baada ya siku mbili ulitokea msiba hukohuko kwao, na alipoenda kule alianza kutambulishwa na mama yake kuwa Jaffarai ni kaka yake na hapo kwenye msiba kulikuwa na dada zake jamaa ambao nao ni dada zake huku mama yake akimwambia walishindwa kuwaambia kwani ni makosa ambayo tayari yalikwisha tokea.

“Utambulisho ule ulinifanya niishiwe nguvu kwa sababu jamaa nilikuwa nashinda naye sana sehemu sehemu na hata yeye hakuwahi kunaimbia ishu hii nahisi alikuwa hajui, lakini hata hivyo nashukuru kwani sasa nimejua mshkaji ni kaka yangu na nafurai sana,” alisema Z-Anto.

Hata hivyo alisema kuwa mama yake na mama yake Jaffarai wanaitana dada hivyo udugu wao si wa kufosi kwani kila kitu kilijulikana katika msiba huo uliowakutanisha na dada zake Jaffarai pamoja watu wengine ambao hakudhania kama waweza kuwa ndugu zake.

  Source

0 comments:

Post a Comment