Mwamitindo
wa kimataifa wa Tanzania Flaviana Matata
jana amepost picha akiwa na Lady Gaga ambaye
hata hivyo sura yake haionekani vizuri kwakuwa anaonekana usoni akiwa amevaa
maua yaliyozungushwa kwenye duara.
Miongoni mwa picha hiyo, kuna picha ambayo anaonekana msanii huyo wa ‘Born This Way’ akimbusu Flaviana Matata. Katika picha hiyo Flaviana ameandika maneno aliyomnukuu Lady Gaga aliyomwambia “thank you for doing my video gal,u killed it”.
Kwa maelezo hayo inaashiria kuwa Flavy ataonekana kwenye video ya msanii huyo mwenye vituko kibao. Flavy yupo mjini London, Uingereza kwenye tamasha la London Fashion Week.
Naye Lady Gaga yupo London kwaajili ya uzinduzi wa perfume yake, FAME ambapo imedaiwa ametumia paundi milioni 1 kwenye uzinduzi huo.

0 comments:
Post a Comment