Saturday, September 8, 2012

'Muziki Haujanilipa' - Enrico

Mtayarishaji mahiri wa Muziki hapa nchini Tanzania, Enrico Figueiro wa studio ya Sound Crafters ametoa lawama nyingi kwa mfumo wa muziki wa Bongo na kusema kuwa haujamlipa kama ambavyo angestahili.

Enrico ambaye kwa sasa amejikita katika utayarishaji wa muziki wa bendi na muziki wa aina tofauti na Bongoflava, amesema kuwa yeye ni moja ya Maprodyuza ambao wamekwishatengeneza ngoma nyingi za muziki wa Bongoflava kushinda watayarishaji muziki wengine wakongwe na wa sasa lakini kimsingi hakuna faida yoyote kubwa ambayo ameweza kujipatia kutokana na hilo.

Enrico ambaye hawezi kusahaulika kwa kufyatua ngoma hits mbalimbali ikiwepo ile ngoma ya Dar Mpaka Moro ya Wanaume TMK, amesema kuwa bado hajaacha kutengeneza muziki wa Bongoflava na kwa msanii yeyote ambaye anajisikia kufanya naye kazi anaweza kuwasiliana naye na kufanyakazi.

0 comments:

Post a Comment