Tuesday, September 4, 2012

'KIRI RECERDS' KUWAIBUA CHIPUKIZI



Wakati baadhi ya studio zikishindwa kufanya kazi na wasanii chipukizi na wale wa ngoma za asili kwa madai kuwa wanasumbua, studio ya Kiri Records, imesema kuwa ipo katika mchakato wa kuwachukua wasanii chipukizi na kufanya nao kazi hasa wale ambao hawajawahi kuingia studio kabisa.

Producer mahiri wa studio hiyo, C9, alidai kuwa wapo wasanii wengi chipukizi ambao wana uwezo mkubwa wa kuimba lakini wanakosa nafasi ya kuonesha uwezo wao kwa kubaniwa kurekodi katika studio mbalimbali nchini.

Alisema uongozi wa studio hiyo umekaa na kuliona hilo ambalo tayari wameanza kulifanyia kazi kwani jukumu lao kama wadau wa muziki na ishu zote za sanaa ni kujaribu kuwatoa wasanii wote wanaoonesha nia ya kufanya kazi.

0 comments:

Post a Comment