Ikiwa ni siku chache
baada ya kutoka kwa wimbo ulioshirikisha wasanii kadhaa wakijiita Mbeya All
Stars, Rapper Izzo Bizness anayewakilisha mkoa wa mbeya amefunguka kuhusu na
kusema hakujua kuhusu hiyo nyimbo wala imetengenezwa wapi na hajahusishwa kwa
lolote.
Izzo amesema hajakataa
kufanya Mbeya All Stars ila kwa sasa huu mziki ni biashara na kila unachofanya
uwe na malengo sio ku copy na kupaste tu.
“Sio sababu flani
wamefanya na sisi tufanye, Kigoma
All Stars wamefanya kitu kizuri na wamesafiri kwenda Kigoma na Wamefanya show pia
wameboresha mambo yao tofauti kupitia udhamini wa hiyo nyimbo, wakati unafanya
Project kama hizi lazima ujue lengo lako na sio kufanya kwa kugeza tu”.
Izzo alisema Tayari
watu wa Mbeya wanajua anachofanya na anawakilisha vizuri kabisa na hilo ni
tosha kabisa kwa mji wake .
0 comments:
Post a Comment