Sunday, September 2, 2012

HEMED AOMBE MSAMAHA WANAWAKE - JACKLINE PENTZEL


Baada ya msanii wa filamu bongo Hemed Suleiman ‘P.H.D’, kutangaza endapo akiamua kuoa basi atafanya mchakato kama wa kufanya usaili kama ilivyo BSS au mashindano mengine ili kufanya mchujo wa mwanamke mzuri atakayekuwa mke wake, kauli hiyo imepingwa na mwanadada Jackline Pantezel ‘Jack wa Chuz’, kwa madai kitendo alichokisema msanii huyo kinahitaji awaombe msamaha wanawake kwani anawafananisha na samaki wanaovuliwa kirahisi.
Kauli ya Jack imeonyesha wazi kuwa anawatetea wanawake na hataki waonekane kama hawana maana yoyote ndani ya jamii au watu wanaokaa na kusubiri kuolewa tu wakati maisha ya sasa hayapo hivyo, na mwanamke yeyote atakaejitokeza kwenye mchakato huo atakuwa hana akili na atakuwa ni kahaba.

“Nilisikia tu kwamba anataka kufanya kitu kama BSS katika kutafuta mwanamke wa kuoa, na hapo ina maana kuwa tayari amesha wafanya wanawake kama samaki,” alidai Pentzel.


Hemed Suleiman 'PHD'

0 comments:

Post a Comment