Showing posts with label Zitto Kabwe. Show all posts
Showing posts with label Zitto Kabwe. Show all posts

Tuesday, December 24, 2013

HAWA NDIYO WANAOMFUKUZA ZITTO NDANI YA CHADEMA

 
Dar es Salaam,Tanzania.
WAKATI sinta fahamu kuhusu sakata la Kamati Kuu ya Cha Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kumfukuza katika safu ya Uongozi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zitto Kabwe,taarifa za ndani ya Chama hicho zinaeleza kwamba Mbunge huyo wa Kigoma amefukuzwa uachama.



Taarifa zinaeleza kwamba ingawa kuna mvutano mkubwa kuhusu kufikia uamuzi huo,ila wajumbe wa Kamati Kuu wamezidia nguvu na Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dk Willbrod Slaa ambao wamegoma katakata kuwasamehe watuhumiwa hao huku wakisema kwamba kitendo cha kuwa samehe itaongeza uhaini ndani ya Chama. 



Inaelezwa kwamba hatua hiyo pia ili sababisha mwasisi wa Chama hicho Mzee Edwin Mtei kuingilia kati suala hilo, lakini akazidiwa nguvu na wawili hao kwa hoja kwamba Zitto akisamehewa Chadema itakufa,hivyo ni bora akafukuzwa ili wabaki na kazi moja ya kukijenga Chama mapema kabla ya kufika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Monday, December 16, 2013

Mbowe amvaa Zitto

Na Benjamin Masese, Mwanza
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amemvaa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na kusema kamwe chama hicho hakiwezi kuvumilia usaliti wa aina yoyote.

Akizungumza mjini hapa jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Malimbe, alisema kwa namna yoyote ile hawatamfumbia macho mtu yeyote anayekwenda kinyume cha katiba na taratibu za chama hicho.

Alisema Chadema ambayo imejengwa kwa damu za Watanzania haiwezi kukubali kuona mtu yeyote anatoboa ‘boti’ yake iendayo kasi katikati ya bahari wakati huu wa kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwakani.

Mbali na kumshukia Zitto pia amekirushia kombora Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kusema kinatumia mbinu chafu kutaka kuiua Chadema kabla ya mwaka 2015.

Alisema kamwe mbinu hizo hazitafanikiwa maana Chadema ipo kwa mpango wa Mungu.

Ingawa Mbowe hakumtaja Zitto kwa jina lakini hotuba hiyo ilionekana dhahiri kumlenga Zitto, Dk. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba waliovuliwa nyadhifa zao zote za uongozi ndani ya chama hicho hivi karibuni.
SOMA ZAIDI: MTANZANIA ONLINE