Msanii wa filamu, Wastara Juma amewaomba Watanzania na wadau mbalimbali
kuungana naye siku ya tarehe 28 December 2013 saa tatu asubuhi makaburini
Kisutu jijini Dar es Salaam kwaajili ya kufanya dua maalum ya Sajuki.
Wastara ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Facebook.
“28 Jumamosi kuanzia saa 3 asubuhi naomba mashabiki wangu na wapenzi wa
kipenzi changu kipenzi chenu Sajuki tukutane kaburini kisutu kwa ajili ya
dua ya pamoja…kwa Dar es salaam lakini dua rasmi ni 2.01.2014 Songea
"..aliandika Wastara.










