Showing posts with label Azamtv. Show all posts
Showing posts with label Azamtv. Show all posts

Monday, December 16, 2013

Uzinduzi AzamTv Leo Desemba 16, 2013

Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media, Yusuf Bakhresa akisalimiana na wasanii wakati wa ufunguzi wa Ofisi ya AZAM TV.Baadhi ya wasanii maarufu nchini wakiwa na Meneja wa Uhusiano wa AzamTV, Maryam El-haj  wakati wa ufunguzi wa Ofisi ya AZAM TV.


DAR ES SALAAM, Tanzania

WASANII wa filamu nchini, wamekiri kufurahishwa kwao na ujio wa kituo cha Teevisheni cha Azam (Azam Tv) na kuutaja kama ukombozi utakaochagiza maendeleo ya sanaa na wasanii ndani na nje ya nchi.

Wakizungumza wakati wa uzinduzi wa Makao Makuu ya Kampuni ya Azam Media Ltd, wasanii hao, Jacob Steven ‘JB’, Mahsen Awadh ‘Dk Cheni’, Yvone Cherry ‘Monalisa’ na Suzan Lewis ‘Natasha,’ walisema kama wasanii wanatarajia mengi yaliyo bora kutoka Azam Tv.

Kwa upande wake JB alisema sanaa ya Tanzania hususani ya filamu na wadau wake, wamepata sehemu muhimu itakayosaidia kukuza sio tu kiwango cha ubora wa kazi zao, bali pia pato la wasanii kutokana kutokana na mikataba ya matangazo ya muvi zao.

“Tuna matumaini makubwa kwamba ujio wa Azam Tv ni moja ya njia zitakazoboresha kazi na pato la wasanii. Ni fursa nyingine ambayo wasanii tunapaswa kuitumia vema ili kuwafikia wadau wetu kupitia,” alisema JB mmoja wa wasanii nguli wa Bongo Muvi.

Monalisa, yeye alibanisha kuwa matarajio ya wasanii wengi ni kuwa ujio huo wa Azam Tv utakwenda sambamba la ongezeko la mikataba ya kurushwa kwa filamu zao, kwani kabla ya hapo kulikuwa na mikataba michache.

“Naamini hii ni moja ya neema miongoni mwa wasanii, lakini kwa sanaa na wadau wake kwa ujumla. Tutapata mikataba minono ya kurushwa kwa filamu zetu hapa na kutanua pato letu. Hakika nimefurahia ujio wa Azam Tv,” alisema Monalisa.

Dk Cheni naye hakuwa mbali na maoni ya wenzake, akisema anaamini fursa ya wasanii kuwafikia wadau na wadau kupata vilivyo bora kutoka kwao imepata kiunganishi muhimu ambacho ni Azam Tv.
“Kwangu mimi Azam Tv ni zaidi ya kituo cha Televisheni. Nakichukulia hiki kama kiunganishi muhimu cha sisi kuwafikia mashabiki wetu, lakini wao pia kutuona kwa mapana na kuchangia maendeleo ya sanaa na wasanii Tanzania,” alisema Dk Cheni.

Natasha yeye kwa upande wake aliupongeza uongozi wa Azam Media kwa kuwajali wasanii kwa kuanzisha chaneli ya Sinema Zetu inayopatikana katika king’amuzi cha Azam Tv na kwamba anaamini itakuwa chachu kuu ya mafanikio ya sanaa nchini. 


AzamTv yazinduliwa rasmi leo

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Azam Media,Yussuf Bahresa akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Televisheni yao ya Azam kwenye makao makuu yao yaliopo Pugu Road,jijini Dar es Salaam leo.

 Mkurugenzi mtendaji wa Azamtv, bwana Yusuf Bakhresa akizungumza na waandishi wa habari leo.
Mkurugenzi mtendaji wa Azamtv, bwana Yusuf Bakhresa akisalimiana na wasanii mbalimbali waliohudhuria katika ufunguzi wa ofisi ya AZAMTV siku ya jumatatu tarehe 16 Desemba 2013

Friday, December 6, 2013

TCRA yaipa Azam Media leseni kuiwezesha kuendesha shughuli zake.

Azam Media Ltd  leo imepata leseni kutoka Mamlaka ya Mawasilino Tanzania (TCRA) na hivyo kuwa na uwezo wa kuanza rasmi shughuli zake hapa Tanzania.
Hatua hii muhimu sasa inaiwezesha AzamTV kuanza kutoa huduma zake kwa wateja wake kote Tanzania kuanzia tarehe16 Desemba. Huduma hii itwapa fursa wateja kuangalia zaidi ya chaneli 50 za kitaifa na kimataifa ziliozosheheni burudani kwa ajili ya familia kwa bei nafuu ya shilingi 12,500/= kwa mwezi. 
Kutakuwepo wigo mpana wa kuchagua kifaacho kuangalia vikiwemo vipindi vya michezo, makala, watoto na tamthilia kutoka Tanzania, barani  Afrika na sehemu mbalimbali za dunia. Baadhi ya vipindi hivyo tajwa vitapatikana katika chaneli maarufu  kama vile National Geographic Gold na Nickelodeon, na pia matangazo yetu yatakuwa na chaneli za bila malipo zikiwemo TBC1, Channel 10, Clouds, ZBC na K24.
Jambo la kusisimu zaidi  ni kwamba  AzamTV itakuwa na matangazo katika chaneli zake tatu:
AzamOne - Itakuwa na vipindi vya kiafrika, ambapo kwa asilimia kubwa vitahusu masuala ya Afrika Mashariki kwa lugha ya Kiswahili. Hii ndiyo chaneli ambayo itakuwa ikirusha matangazo ya Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara;
AzamTwo – Hapa vitapatikana vipindi vya burudani kwa familia amabavyo ni vya kimataifa na baadahi ya hiovyo vitakuwa katika lugha ya kiswahili;
SinemaZetu – Chaneli maalum kwa ajili ya tamthilia za kitanzania.
Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington, alisema: “Huu ni  wakati wa kujivunia  kwa Tanzania kwani sasa ina huduma za luninga zinazopatikana kwa  bei ambayo wengi wanaweza kuimudu.  Miezi michache ijayo tutaivusha huduma hii mipaka hadi katika nchi zingine za Afrika Mashariki na hata mbali zaidi. Nimefarijika kwamba tumewekeza vilivyo katika chombo hiki cha kitanzania na tutaendelea kufanya hivyo”.
Torrington pia alibainisha kuwa kwa wateja ambao hawatapenda kungojea kuzinduliwa rasimi wa huduma za Azam TV, milango ya ofisi zake za Dar es Salaam itakuwa wazi kuanzia  leo (Ijumaa Desemba 6, 2013).  Wateja wataweza kununua  vifaa muhimu kutoka duka la AzamTV na kwa mawakala walioidhinishwa  na hivyuo kuweza kujionea vipindi mbalimbali kuanznia sasa – japo malipo yao kwa mwezi yatahesabiwa kuanzia Desember 16.