Kwa mujibu wa Young D mwenyewe anasema hakuwa amepanga kutoa video hiyo mapema ila alikuwa amelenga kuitoa siku atakayokuwa na furaha sana.
Baada ya kupokea taarifa za msanii mwenzake Dogo Janja kumpoteza baba yake mzazi Abubakari Chende ndio alipoamua kuitoa hii video kama dedication kwa Dogo Janja, kupitia instagram account yake Young D kaandika ujumbe huu.
“Nilipanga kuachia video yangu nikiwa na furaha sana. Furaha yangu nilitamani sana itawale kwanzia kwangu, mashabiki wangu, pamoja na wasanii wenzangu. Bahati mbaya msanii mwenzangu @dogojanjatz amepoteza nguzo imara sana katika maisha yake”.
“Miaka 8 iliyopita nilipitia changamoto kama hiyo kwa kumpoteza mzee wangu. Kitu pekee nilichokua nahitaji ni FURAHA itokanayo na faraja kutoka kwa watu walionizunguka. Nilikua sina mpango wowote wa kuachia wimbo wangu wiki hii”
“Lakini nimeamua kuachia Video ya wimbo wangu leo, kama Dedication kwa @dogojanjatz. Wimbo wangu unaitwa FURAHA. Naamini ni nguzo pekee anayoihitaji Mwanangu Janjaro kwa sasa. You Have all my Support Young Badman, I have Nothing But Love to You”
0 comments:
Post a Comment