Msanii wa muziki wa R&B, Benard Paul ‘Ben Pol’, yupo katika
maandalizi ya mwisho ya kuachia albamu yake aliyoipachika jina la
mwanaye wa kwanza, ‘Mali’ aliyezaliwa hivi karibuni.
Akizungumza na gazeti la Mtanzania, Ben Pol amesema albamu hiyo itatoka katikati ya mwezi wa sita.
“Nimefanikiwa kukamilisha albamu yangu bila msaada wa mtu mwingine
yeyote ndiyo maana nimeamua kuiita jina la mwanangu, ‘Mali’. Kwa sababu
kila kitu nimefanya mwenyewe na kuenzi jina la mwanangu,” alisema Ben
Pol.
Pia Ben Pol alisema kabla ya kuachia albamu hiyo anatarajia kuachia
video ya wimbo ‘Moyo’ akiwa ameifanyia nchini Afrika Kusini chini ya
mtayarishaji, Lolpop katika studio ya Tetemesha.







0 comments:
Post a Comment