Friday, August 7, 2015

Haya ndiyo majina ya wasanii yaliyopo kwenye picha aliyopewa zawadi Rais Kikwete

jk2
Rais Jakaya Kikwete
Muungano wa wasanii Tanzania August 06 walikutana na Rais Jakaya Kikwete pamoja na Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dkt John Magufuli kwa ajili ya chakula cha usiku pamoja na kuzungumza kuhusu sanaa ya Tanzania.
jk11
Rais Jakaya Kikwete pamoja na Dkt.Magufuli.
Hii iliwahusu wasanii wa Filamu na muziki ambao kwa pamoja waliamua kumkabidhi Rais Jakaya Kikwete zawadi ya picha yake ikiwa na majina ya wasanii wote wa Tanzania,picha hiyo niliinasa pia mtu wangu ni hii.
typo2
Picha aliyozawadiwa Rais Kikwete yenye majina ya wasanii.
Ukiangalia vizuri picha hii utaona majina ya mastaa wako kadhaa kama Madee,Wema Sepetu,Mwasiti,Young Killer,Vanessa Mdee,Juma Nature,Matonya,Mwana Fa,Barnaba,Mo Music,Damian Soul,Jokate,Afande Sele,Ommy Dimpoz,Yamoto Band na mengine mengi

0 comments:

Post a Comment