Mwanamuziki wa muziki wa dansi aliyepata kushika
chati za juu katika utunzi na uimbaji katika bendi mbalimbali nchini za muziki
wa Dansi , Ramadhani Masanja 'Banza Stone' amefariki
dunia hii leo mchana nyumbani kwao Sinza Kijiweni Dar es Salaam.
Nyota huyo wa zamani wa bendi hiyo ya Twanga
Pepeta na Tot alikuwa akiumwa kwa muda mrefu.
Mmiliki wa Bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka
amethibitisha kifo cha Banza Stone.
"Ni kweli amefariki leo mchana saa saba,
baada ya kutoka msikitini ndiyo tumepata taarifa hizo za msiba," alisema
Asha Baraka.
0 comments:
Post a Comment