Baadhi ya watu
wanahisi kuwa uchunguzi zaidi unahitajika
Uchunguzi wa
utafiti kutoka chuo kikuu cha Exeter nchini Uingereza, unaonyesha kuwa kiwango
cha mbegu za uzazi za wanaume huathiriwa kwa kuweka simu za mkononi kwenye
mifuko ya suruali.
Hata hivyo
,mwana sayansi wa maswala ya uzazi na shahawa,alisema kuwa ushahidi huo bado haukuwa
na uhakika wowote hivyo basi simu yake bado inaendelea kukaa mfukoni mwake.
Uchunguzi huo
uliochapishwa katika jarida la 'Environment International' ulilaumu mnunurisho
wa kielectromagnetiki kuwa chanzo kikuu.
Lilichanganua
tafiti kumi tofauti kuonyesha ubora wa shahawa ikihusisha wanaume 1,492.Hii
ilijumuisha kupimwa kwa shahawa zilizowekwa wazi kwa mnunurisho wa simu za
rununu, kwa maabara na udadisi wa wanaume katika cliniki za uzazi
Kiongozi wa
uchunguzi huo Dkt.Fiona Mathews aliambia BBC kuwa kutokana na uchunguzi
huo,moja tu ndio ulionyesha uhusiano kati ya utumizi wa simu na kudidimia kwa
ubora wa shahawa.
| Mbegu za uzazi za wanaume zinasemekana kuathirika kutokana na simu za mkononi |
"Nafikiri
kwa mwanamume wa makamu hakuna haja ya kuingiwa na hofu,iwapo unajua una
uwezekano wa kuwa na shida ya kizazi basi itakuwa jambo la busara kutoweka simu
mfukoni ,pia kugeuza mtindo wako wa kula."
'Uchunguzi
zaidi'
Alikubali
kukosolewa na wana sayansi wengine huku akiunga mkono kuwa kuna umuhimu wa
kufanya uchunguzi zaidi.
Dkt,Mathews
alimaliza kwa kusema"hili ni jambo la kusisimua lakini hatusemi kwa
uhakika kuwa kila anayebeba simu mfukoni atakuwa na shida ya kizazi."
Dkt.Allan Pacey
kutoka chuo kikuu cha Sheffield anasema kuwa wazo hilo la kudidimia kwa shahawa
na kuharibu "DNA"linatokana na "radio frequency" na
mnunurisho wa kielectromagnetiki zinazopatikana kwenye simu na pengine joto
aidha moja kwa moja kutoka kwenye simu au mnunurisho.
Dkt huyo
anayefanya uchunguzi wa shahawa bado hajashawishika akisema ushahidi huo hauna
msingi na ataendelea kuweka simu mfukoni.
Aliambia
BBC,"kumekuwa na shauku kwa mda kama kuweka rununu mfukoni kunaweza
changia kudidimia kwa ubora wa shahawa na nguvu za kiume kivyovyote.
"Kumekuwa
na habari zisizokuwa na msingi lakini kwa maoni yangu uchunguzi uliofanywa hadi
kufika sasa haujakuwa wa kutosha kwa sababu wachunguzi aidha hawakuhifadhi
shahawa vile inavyofaa ama wamedadisi matumizi ya simu kati ya wanaume bila
kuzingatia mambo mengine kama mitindo yao ya maisha.
"Tunayohitaji
ni uchunguzi kufanywa ambapo utumizi wa simu unazingatiwa vile vile tabia
zinazoathiri maisha yao.
Hadi pale
tutakapo tafakari hayo,nitaendelea kuweka simu yangu katika mfuko wa mkono wa
kulia wa suruale yangu!"







0 comments:
Post a Comment