Baadhi ya waandishi wa habari na wadau kutoka asasi mbalimbali
nchini wakifanya usajili kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa
kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini
Arusha.(Picha na Zainul Mzige).
Na Waandishi Wetu, Arusha
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda ametoa wito
kwa waandishi wa habari nchini kuyapa uzito matukio yanayowatokea
waandishi wa habari na kuyapigia kelele kwa nguvu zote ili kuyakomesha.
Kibanda aliyasema hayo jana mjini Arusha katika kongamano
lililoandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya
habari duniani na kuongeza kwamba wakati umefika kwa waandishi wa
habari kuondoa tofauti zao na kuungana pamoja kuongeza nguvu waliyonayo
kukabiliana na ukatili unaoendelea dhidi ya waandishi wa habari katika
miaka ya hivi karibuni.
“Baadhi ya wahariri huwa hawayaandiki madhila yanayowasibu waandishi
wa habari na kuyapa uzito unaostahili aidha kwa huyapuuzia au kudharau
kwa kuwa hayawahusu moja kwa moja,” alisema Kibanda.
Aliongeza kwa kusema kuwa vyombo vya habari mara nyingi vimekuwa
vikinyooshewa vidole na kulaumiwa kwa kutokufanya kazi kwa uadilifu
jambo ambalo linatafsiriwa kuwa ni la uonevu, vinatumiwa vibaya na
hakuna anayesimama kuvitetea kutokana na mchango wake mkubwa katika
jamii.
Afisa Mipango Kitengo cha Mawasiliano, Habari na Tehama UNESCO,
Bw. Al Amin Yusuph, akiwasilisha mada kuhusu mchango wa uhuru wa vyombo
vya habari katika utawala bora, kukuza uwezo na kupunguza umaskini
kongamano la waandishi wa habari lilioandaliwa kama sehemu ya
maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yanayofanyika
jijini Arusha.
“Kwa sasa tasnia hii iko kwenye wakati mgumu sana kwani hata marais
wa nchi mbalimbali mfano Uganda, Kenya hata Marekani wanakinzana na
vyombo vya habari kwa madai kuwa kauli zao zinapotoshwa, laikini ukweli
ni kwamba ni vyema kauli hizo za viongozi zikachunguzwa kwa undani zaidi
ili kuelewa iwapo zina uwajibikaji ndani yake,” alisema Kibanda.
Kibanda aliongeza kuwa wakati umefika sasa kwa waandishi kutambua
kuwa kuna ajenda za siri zilizojificha dhidi ya uteswaji wa waandhishi
wa habari hivyo yasidharauliwe, yafanyiwe kazi kwa kina ili kuelewa
kiini cha tatizo kwa kupata ufumbuzi.
Kwa upande wake mwandishi mkongwe na aliyetunukiwa tuzo ya maisha
mwaka 2012 na Baraza la Habari Hamza Kasongo alisema vyombo vya habari
vina nguvu kubwa katika kushawishi hivyo vitumie nguvu hiyo kama
muhimili wa nne wa nchi katika kuzikabili changamoto zilizopo.
“Kuwe na mtandao unaoeleweka wa mawasaliano kati ya waandishi wa
habari nchini ili kuhakikisha kuwa matatizo yaliyopo yanatatuliwa bila
woga na kwa ujasiri kwa lengo la kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa,”
alisema Kasongo.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Sheria , Bw.
James Jesse, akitoa mada kuhusu umuhimu wa sheria katika kulinda haki ya
uhuru wa kujieleza kwa kila mtu wakati wa kongamano la waandishi wa
habari lilioandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa
vyombo vya habari duniani yanayofikia kilele leo jijini Arusha.
Mwanahabari mwingine mkongwe Dokta Samwilu Mwaffisi aliyetoa mada ya
Maadili ya Uandishi wa Habari alisema kuwa kuna haja ya waandishi
kuzingatia uhuru wa habari walionao kwa kuzingatia maadili
yanayowaongoza ili kuboresha heshima waliyonayo katika jamii kwa
kuandika ukweli na uhakika, bila upendeleo, kutoa fursa ya kujitetea na
kukubali kuomba radhi pale unapokosea.
“Kuandika habari zenye kuzingatia maadili kunapunguza manung’uniko,
mashauri na kuongeza heshima ya chombo cha habari na mwanahabari
mwenyewe,”
Akizungumzia suala la ufanisi, Rais wa Vilabu vya Waandishi wa
Habari, Kenneth Simbaya, aliwaasa waandishi wa habari kusimamia ukweli
katika kazi zao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea jambo ambalo
litakawaweka huru zaidi katika utekelezaji wa shughuli zao za uandishi
wa habari.
Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na umoja wa asasi mbalimbali chini ya
uenyekiti wa MISA TANZANIA unafikia kilele chake tarehe 3 Mei kwa
kuzindua majarida mbalimbali, matamko kutoka asasi mbalimbali na
kuhitimishwa kwa tafrija ya chakula cha jioni chini ya mgeni rasmi Jaji
Mstaafu Mheshimiwa Mark Bomani.
Mwanahabari Mkongwe kutoka Chuo Kikuu Huria, Dokta Samwilu
Mwaffisi (kulia) akiwasilisha mada ya Maadili ya Uandishi wa Habari
kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo
vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha. Kushoto ni Mhadhiri
kutoka Chuo Kikuu cha Iringa, Bw. Simon Berege.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda, akitoa
maoni yake wakati wa kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha
Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
Pichani juu na chini ni baadhi ya waandishi wa habari wakongwe,
mabalozi na wanahabari washiriki katika kongamano la siku moja
lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014
lililofanyika jijini Arusha.
Mwandishi wa Habari Chokonozi, Bw. Fredrick Katulanda, akielezea
madhila mbalimbali yaliyomsibu katika utekelezaji wake wa kuandika
habari za uchambuzi.
Mwanahabari Mkongwe Bi. Leila Sheikh akichangia mada ya Mchango wa
Uhuru Wa Vyombo Vya Habari Katika Utawala Bora, Kukuza Uwezo Na
Kupunguza Umaskini wakati wa kongamano la siku moja lilioandiliwa
kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini
Arusha.
Mmiliki wa Gazeti tando la Mjengwa na Kituo cha Redio Kwanza
Jamii, Bw. Maggid Mjengwa akielezea jinsi Intaneti inavyoweza
kuunganisha mtandao wa Redio.
Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania
(COMNETA) na Mkurugenzi wa kituo cha mawasiliano Sengerema, Bw. Felician
Ncheye akichangia mada.
Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose Haji Mwalimu, (kushoto) akiwa na baadhi ya washiriki wa Kongamamo hilo.
Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth Simbaya, akishiriki kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
Picha juu na chini Baadhi ya washiriki wakichangia maoni yao
kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo
vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
Kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 likiendelea.
Mwanakamati wa maandilizi ya maadhimisho ya Kongamano la Uhuru wa
Vyombo vya Habari Duniani 2014, Usia Nkhoma Ledama wa Kitengo cha Habari
cha Umoja wa Mataifa (UNIC), akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda nje ya ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa AICC jijini Arusha.







0 comments:
Post a Comment