Wednesday, May 14, 2014

KINANA AKAGUA UJENZI WA MAJENGO MBALIMBALI MAKAO MAKUU YA WILAYA YA UYUI, TABORA

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinan  (katikati),  akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Wilaya ya Uyui, Steven Nanda (kulia) alipotembelea Makao Makuu ya Wilaya ya Uyui, Tabora, kukagua ujenzi wa nyumba za watumishi, jingo la wilaya hiyo, kituo ca polisi na jingo la halmashauri.Kshoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Uyui, Mussa Ntimizi.


Na Richard Mwaikenda,Uyui,Tabora

KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, ametaka Halmashauri za wilaya nchini, kutenga viwanja vitakavyotolewa bure kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), likalojenga nyumba za gharama nafuu watakazouziwa watumishi wa umma kwa bei nafuu.


Amesema endapo halmashauri zitaendelea na mtindo wake wa kulizuzia shirika hilo viwanja kwa bei kubwa, basi wajue kwamba wanaowakomoa ni watumishi, kwani gharama hiyo itaongezwa kwenye bei ya nyumba, hivyo kitendo hicho kuwaumiza watumishi.

Kinana alizungumza hayo baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba 50, katika makao makuu ya wilaya hiyo, na kuelezwa na  alilezwa na Meneja wa NHC Mkoa wa Tabora, Erasto Chilambo kuwa eneo walilojenga nyumba hizo wameuziwa kiwanja kwa sh. mil. 51, hivyo kuongeza gharama ya ujenzi hivyo kuzifanya nyumba hizo kuuzwa kwa bei kubwa.

Ndugu Kinana alihidi kulifanyia ufumbuzi tatizo hilo, kwa kulizungumzia katika vikao vya juu vya chama hicho, ikiwemo Kamati Kuu.

KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana leo katika mwendelezo wa ziara yake wilayani Uyui, amekagua Makao Makuu ya wilaya hiyo kwa kukagua miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi wa Serikali, chanzo cha maji, ujenzi wa  jengo la polisi pamoja na ujenzi wa nyumba 50 za bei nafuu zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)ibu Mkuu.

Katika makao makuu ya wilaya hiyo yaliyopo Isikisya,  pia kuna miradi kuna mwendelezo wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya na majengo ya Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa alimweleza Katibu Mkuu, Ndugu Kinana kuwa asilimia kubwa ya miradi hiyo, inajengwa kwa kutumia fedha zinazotokana na vyanzo vya ndani vya halmashauri hiyo.

Mwassa alisema kuwa wakati anateuliwa kuwa Mkuu wa mkoa huo, akitokea Wilaya ya Mvomero, Mkoani Morogoro alikokuwa Mkuu wa Wilaya, alikuta eneo la Makao makku ya Uyui  hakuna miradi inayoendelea na kwamba asilimia kubwa ilikuwa ni vichaka, lakini baada ya kuanza kazi ilibidi akae kikao na madiwani kujadili ni namna gani wataendeleza makao makuu hao. Wilaya ya Uyui itangazwa na Rfais Benjamini Mkapa mwaka 2004.

Katika kikao hicho Mwassa aliwapa ushauri madiwani kwenda kujifunza Mvomero jinsi ya kuiendeleza halmashari hiyo, jambo ambalo walilikubali na kwenda huko na hatimaye matunda yake ndiyo kama yanavyoonekana sasa  Uyui.

Baada ya hapo msafara ulielekea Ilolangulu, ambapo Katibu Mkuu, Kinana alikagua maabara, vyumba vya  madarasa katika Shule ya Sekondari ya Ilolangulu ambapo yeye na viongozi wengine akiwemo Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, walipanda miti katika eneo hilo la Shule.

Baada ya hapo Kinana aliongoza mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya ya Uyui na kusomewa na Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Lucy Mayenga taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM, pamoja na kusomewa taarifa ya uhai wa chama.

0 comments:

Post a Comment