GARI la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe,
limekamatwa na kuendelea kushikiliwa mjini Mombasa nchini Kenya,
kutokana na kuwa na namba mbili.
Taarifa kutoka Kenya zilizolifikia gazeti hili jana, zilieleza kuwa
polisi nchini Kenya walipata taarifa za kuwepo kwa gari hilo na watu
ambao walionekana kutokuwa na kazi maalumu.
Baada ya kupata taarifa hizo, Polisi hao walio katika msako wa wageni
na magari yanayotiliwa shaka kuhusika katika uhalifu na ugaidi,
walianza kulifuatilia na kubaini wahusika wa gari hilo.
Ufuatiliaji huo kwa mujibu wa taarifa hizo, ulibaini wahusika wa gari
hilo walipofika Mombasa kutokea Tanzania, hawakuonekana kupokewa na
mwenyeji yeyote, hali inayomaanisha wenyewe ni wenyeji wa mji huo.
Taarifa za Polisi zilibainisha kuwa uchunguzi wao ulibaini kuwa gari
hilo liliwabeba Mbowe, Mbunge wa Mwanza Mjini, Ezekiah Wenje na dereva
Ibrahim Nguzo.
Polisi hao inadaiwa walitilia shaka gari hilo kutokana na kuwa na
namba za usajili STK 8146, ambazo zilipandishiwa juu ya nambari halisi
za gari hilo ambazo ni KUB.
Uchunguzi wa Polisi hao ulibaini kuwa Mbowe na Wenje waliwasili
Mombasa, Kenya kwa gari wakitokea Tanzania kupitia mpaka wa
Horohoro/Lungalunga na kwenda moja kwa moja hotelini.
Mashaka kwa Polisi hao yaliongezeka baada ya Mbowe na Wenje Aprili 26
mwaka huu kusafiri kwenda Nairobi kwa ndege, na kumwacha dereva pamoja
na gari hotelini.
Kutokana na hali hiyo, Jumatatu wiki hii saa 5.00 asubuhi askari
Polisi wa Mombasa walimkamata Ibrahim pamoja na gari hilo, baada ya
kuonekana amekaa hotelini muda mrefu bila ya shughuli zozote.
“Hapo ndipo alipotoa habari kwamba alikuwa akiwasubiri wakubwa zake
ambao walikwenda Nairobi tangu Aprili 26 na hawakuwa wamerejea,”
ilieleza taarifa hiyo.
SOMA ZAIDI: HABARILEO ONLINE







0 comments:
Post a Comment