Pichani: Kutoka Kushoto; Profesa Jay, Adam Kuambiana, JB na Q Chillah
Msanii wa Bongo Flava ambaye anajihusisha pia na uigizaji, Q Chief au
Chillah ambaye alikuwa mmoja kati ya watu waliokuwa location na
Marehemu Adam Kuambiana wakishuti filamu ya ‘Jojo’, ameelezea
kilichotokea kabla ya kifo cha Adam Kuambiana.
“Tulikuwa kambini tunashuti movie yake mpya ambayo inaitwa Jojo,
movie ambayo yeye mwenyewe alikuwa anasema itakuwa ni movie ya mwisho
kwake. Ni movie ya mwisho kwa muda huu na atakaa kama miaka mitatu
kuangalia vitu vingine halafu atarudi. Atakuwa tu ana-direct hatocheza.”
Q Chillah amekiambia kipindi cha Hatua Tatu cha 100.5 Times Fm.
Ameeleza kuwa tayari walikuwa wameshashuti filamu hiyo Bagamoyo,
Iringa na muda huo walikuwa Dar es Salaam ambako walikuwa wanashuti
scene za mwisho.
“Leo asubuhi tulikuwa tunaingia location pale biashara complex.
Na wakati tunaingia location mimi najitayarisha kuoga. Assistant
director wa Adam ambaye anaitwa Muxin, akanipigia simu ‘bana Adam yuko
hotelini, yuko chumbani huku lakini simuelewi’. Mimi naingia nakuta Adam
yuko Chooni anaharisha. Tukajitahidi kumwagia maji lakini anaahisha
damu.”
Ameeleza kuwa waliamua kumbeba na kumkimbiza hospitali ya kwanza ambayo walikataa kumpokea kutokana na hali yake.
“Tukasema tutoke twende hospitali ya pili. Tumeenda private, kufika
private daktari anamuangalia within 10 minutes tunajaribu kutafuta simu
kupigia mkurugenzi wetu, kuwapigia watu wa Bongo Movies najaribu namba
ya JB kumbe hayupo…Doctor anasema ‘huyu mtu hatuko nae tena, mwili
umeacha roho’.” Q Chillah amesimulia kwa majonzi.
Ameongeza kuwa kuna filamu nyingi sana Tanzania ambazo jina la Adam
Kuambiana limesaidia kuzikamilisha na kwamba tasnia ya filamu imepoteza
mtu muhimu sana.
Mwili wa marehemu Adam Kuambiana anatarajiwa kupumzishwa kwenye makazi ya kudumu Jumanne (May 20,2014).
Credit: Timesfmradio
Credit: Timesfmradio
Msikilize hapa Q Chillah:







0 comments:
Post a Comment